Kilichomkuta Muna Love kinasikitisha

Kilichomkuta Muna Love kinasikitisha

Moja ya story inayoendelea kutrend katika mitandao ya kijamii ni ya mwanadada Muna Love ambaye hivi karibuni alifanya Surgery ya kutengeneza shape katika mwili wake.

Hata hivyo mwanadada huyo ameibuka katika mitandao na kuonekana kujutia kile alichokifanya na kuwataka watu hasa wanawake wasithubutu kufanya surgery.

Munalove amesema anajutia kufanya surgery na kudai kuwa kuna vitu vingi anapitia na hivyo kuwaomba watu wasifanye.

“Achaneni na Surgery, msifanye nitakuja kuwaeleza vitu vingi ninavyopitia, nampenda sana Yesu,” amesema Muna Love

Itakumbukwa kuwa mwaka jana Muna Love alifanya Surgery ya Dimpoz na umbile hali iliyosabbaisha sasa kupitia wakati mgumu na kulazwa hospitalini.

Maneno ya Muna yamewaibuka mashabiki zake ambao tangu awali walikuwa wakimshauri kutofanya surgery hiyo kwakuwa yeye ni mlokole na anamwamini Mungu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags