Kilicho mkuta Lomalisa uwanjani

Kilicho mkuta Lomalisa uwanjani

Inadaiwa kuwa 'beki' wa kushoto wa ‘klabu’ ya Yanga, Joyce Lomalisa atakuwa nje ya uwanja kwa kati ya siku tano hadi saba akiuguza jeraha alilopata baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa ‘klabu’ ya #Namungo #HashimManyanya.

Aidha Daktari wa ‘timu’ hiyo Moses Itutu amesema 'beki' huyo amepata jeraha eneo la paja kutokana na mchubuko, japo sio tishio.

 Ingawa mchezaji huyo amefunguka kuwa hakufikiria angefanya kitu kama kile ndiyo maana alienda kwa lengo la kuuchukua mpira lakini badaaye aliona mchezaji mpinzani wake anakuja vibaya akidai alimuumiza sana.

Aliendelea kueleza mchezaji huyo alitamani kuendelea kucheza mpira ingawa alikuwa anasikia maumivu lakini baadaye akashindwa kabisa na akaomba kutoka nje ya uwanja, ingawa mpaka anatoka nje ya uwanja bado ‘timu’ yake ilikuwa haijapata bao na akidai ‘mechi’ ilikuwa ngumu, aliumia kuona ana shindwa kuendelea na mchezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags