Kikongwe anayeutikisa ulimwengu wa mitindo

Kikongwe anayeutikisa ulimwengu wa mitindo

Kama umeshawahi kukutana na picha za kikongwe huyo na ukajidanganya kuwa huenda zikawa ni picha zilizotengenezwa na AI (Akili Bandia), basi utakuwa unajidanganya kwani huyu ni mwanamitindo mzee ambaye anaishi ndoto za mjukuu wake.

Kwa majina kamili anajulikana kama Margret Chola maarufu ‘Legendary Glamma’ mwenye umri wa miaka 85 akitokea katika kijiji cha Mashambani kilichopo nchini Zambia kwa sasa ameuteka ulimwengu wa mitindo duniani kote kufuatia na mitupio yake anayovaa.



Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa wazo la kikongwe huyo kujiingiza katika mitindo limetokana na mjukuu wake Diana Kaumba ambaye ni mbunifu wa mitindo anayeishi New York.

Kupitia mahojiano yake aliyoyafanya miezi michache iliyopita Legendary Glamma alieleza kuwa anajihisi amezaliwa upya kupitia mavazi hayo.

“Naji feel tofauti, najihisi mpya na hai katika mavazi haya, kwa namna ambayo sija wahi kuhisi kabla, Najihisi kama naweza kushinda dunia,” alisema kikongwe huyo

Aidha awali alikuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kumfurahisha mjukuu wake lakini alikasirishwa sana baada ya kugundua kuwa anatambulika duniani kote.
“Iliniudhi kusikia kwamba watu wengi duniani wananishabikia, lakini Sasa naweza kuamka nikiwa na kusudi, nikijua kwamba watu duniani kote wanapenda kuniona” alisema Legendary Glamma


Kwa mujibu mwa mjukuu wake Diana alianza kuweka picha za bibi yake huyo katika mitandao ya kijamii (Instagram) mwaka 2023 huku akiuita mtindo huo Granny Series ambapo alipokelewa kwa ukubwa huku akianza kupata madili Aprili 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags