Kijana wa miaka 35 aoa bibi wa miaka 70

Kijana wa miaka 35 aoa bibi wa miaka 70

Kijana Naeem Shahzad mwenye umri wa miaka 35 kutoka nchini Pakstani afunga ndoa na bibi wa miaka 70.

Inaelezwa kuwa wawili hao walikutana katika mtandao wa FaceBook wakati Neem akiwa nchini Canada, ndipo walianzisha urafiki na kisha baadaye kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ambayo kwa mwanzo waliyafanya kwa siri.

Inadaiwa kuwa kijana huyo alishindwa kuficha siri na kuamua kuweka wazi mahusiano yao kwa lengo la kutaka kufunga ndoa na bibi huyo wa miaka 70.

Naeem alifunga safari kutoka Canada hadi Pakstani kufunga ndoa na mpenzi wake huyo, ambaye kwa sasa wamekuwa mume namke.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags