Kijana wa miaka 13 mwenye Kampuni Azua Gumzo

Kijana wa miaka 13 mwenye Kampuni Azua Gumzo

Moja ya stori inayobamba huko mitandaoni ni ya kijana wa miaka 13 kutokea nchini Uingereza Omari McQeen ambaye imeelezwa anatengeneza mkwanja mrefu kupitia mitandao ya kijamii.

Omari McQueen anatengeneza mkwanja huo kupitia mitandao ya kijamii kwa kutengeneza video za mapishi, pia kipindi chake cha 'What’s Cooking Omari?' kinaruka kupitia channel ya watoto ya BBC kwa msimu wa pili.

Imeelezwa kuwa kijana Omary alifundishwa kupika na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka 7, alipofika miaka 10 aliomba wazazi wake ajiunge na mtandao wa LinkedIn, baadae akajiunga YouTube na kuanza kutengeneza maudhui hayo.

Kitendo cha kijana huyo kimewafurahisha wazazi wengi huko mitandaoni na kusema ni kijana anayepaswa kuigwa kwa utendaji kazi na ubunifu wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags