Kijana anayejitambua na mwenye mafanikio ni yupi

Kijana anayejitambua na mwenye mafanikio ni yupi

Na Swaum Mkumbi 

Hey! Guzy mambo zenu, najua ni mgeni katika harakati hizi za kuelimishana kuhusiana na mambo mbali mbali ya vijana na wanachuo, kwa majina naitwa Swaum Mkumbi sasa leo naelezea kuhusu uthubutu wa kijana katika kukabiliana na changamoto ili kufikia malengo yake kama Kijana anayejitambua na mwenye kiu ya mafanikio.

Uthubutu ni uwezo wa kuchukua hatua za kipekee na za ujasiri katika kukabiliana na changamoto.

Kijana anayejitambua na mwenye mafanikio ni mtu ambaye ana uwezo wa kuonyesha uthubutu katika maisha yake, kwa maneno mengine, kijana huyu ana ujasiri wa kutosha kuchukua hatua za kipekee katika maisha yake ili kufikia malengo yake. 

Vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kufikia malengo yao na moja ya changamoto kubwa ni kukosa ujasiri wa kuchukua hatua za kipekee katika maisha yao.

 Vijana wengi hawana uhakika wa nini wanataka katika maisha yao na hivyo hawawezi kufikia malengo yao, wakati mimi Swaumu nafikiria nini nifanye kufikia malengo yangu nilihisi kuwa sitoweza kwasababu sina pesa ila si kweli kuna baadhi ya ndoto zako kuzifikia hazihitaji pesa bali mda wako na kujitoa kwako.

Changamoto nyingine ni kukosa msaada na ushauri kutoka kwa watu wenye uzoefu na ujuzi zaidi kuliko wao. Kwasababu hii vijana wanaweza kukosa mwelekeo sahihi na kuishia kufanya maamuzi yasiyofaa.

Mimi nilikosa ushauri sahihi kutoka kwa watu kwasababu kila mtu alinishauri jinsi anavyotaka yeye lakini mimi nilikuwa na wazo jingine ambalo nikimuelezea mtu anaona nitajichosha tu.

Vijana pia wanakabiliwa na changamoto ya kukosa uwezo wa kujitambua. Wengi wanaweza kutokuwa na ufahamu wa sifa zao za kipekee, udhaifu wao na mambo ambayo wanapenda kufanya. Hii inaweza kuwafanya washindwe kuweka malengo sahihi na kufikia mafanikiona hili ni suala nalolia nalo kila siku vijana tunahitaji sana elimu ya kujitambua.

Kukosa uvumilivu na subira hii nayo ni changamoto ambapo vijana wengi wanataka mafanikio haraka na hivyo hawako tayari kuweka juhudi na uvumilivu ili kufikia malengo yao, tukumbuke kuwa mabadiliko yoyote hayafanyiki kwa usiku mmoja ni mchakato wa muda mrefu kwahiyo yatupasa tuwe wavumilivu. 

Licha ya hayo changamoto nyingine ni kukabiliana na mabadiliko ya ghafla katika maisha yao. Vijana wanaweza kupoteza ajira yao au kukabiliwa na changamoto nyingine ambazo zinaweza kuathiri malengo yao hivyo wanahitaji ujasiri na utayari wa kukabiliana na changamoto hii. 

Kuna mambo kadhaa ambayo kijana anayejitambua na mwenye mafanikio anapaswa kuzingatia

Kwanza, ni muhimu kwake kuwa na malengo wazi na yenye kutekelezeka. Malengo haya yanapaswa kuwa ya muda mfupi, wakati na mrefu. Kwa mfano, kijana anaweza kuwa na malengo ya kupata alama nzuri katika mtihani wake wa mwisho wa shule, kupata ajira bora baada ya kuhitimu au hata kuwa na biashara yake mwenyewe. 

Pili, ni muhimu kwake kuwa na ujasiri wa kutosha kufanya maamuzi sahihi, kijana anayejitambua na mwenye mafanikio anapaswa kuwa na uwezo wa kuamua jambo la kufanya katika maisha yake bila kuogopa kushindwa. Hii inamaanisha kwamba anapaswa kuwa tayari kujifunza kutokana na makosa yake na kuendelea kusonga mbele.

Tatu, kijana anayejitambua na mwenye mafanikio anapaswa kuwa na uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine. Hii inamaanisha kwamba anapaswa kuwa na uwezo wa kupata ushauri na msaada kutoka kwa watu wenye ujuzi na uzoefu zaidi kuliko yeye. Kwa mfano, anaweza kuomba ushauri kutoka kwa wazazi wake, walimu, marafiki au hata wataalamu wa fani yake.

Nne, ni muhimu kwake kuwa na uwezo wa kujitambua, kijana anayejitambua na mwenye mafanikio anapaswa kuwa na uwezo wa kuelewa vizuri sifa zake za kipekee, udhaifu wake na pia mambo ambayo anapenda kufanya. Hii itamsaidia kujua ni nini anapaswa kufanya ili kufikia malengo yake.

Tano, kijana anapaswa kuwa karibu na imani yake ya dini yaani kumshirikisha Mungu kwenye kila hatua kama vijana wa mtaani wasemavyo “kila hatua,dua”hivyo hatua za vijana zinahitaji sana dua na sala za kutosha kwasababu hatuwezi pekeyetu bila kufata sheria pia za dini maana ndipo heshima ilipozaliwa. 

Bila kusahau hii, kijana anayejitambua na mwenye mafanikio anapaswa kuwa na uwezo wa kuishi katika mazingira ya kubadilika. Hii inamaanisha kwamba anapaswa kuwa tayari kubadilika na kukabiliana na mabadiliko ya ghafla katika maisha yake. Kwa mfano, anaweza kupoteza ajira yake au hata kupata fursa ya kipekee ya kufanya kitu kipya.

Kwa kumalizia, kijana anayejitambua na mwenye mafanikio ni mtu ambaye ana uwezo wa kuonyesha uthubutu katika maisha yake. Kwa kufuata mambo haya muhimu, kijana huyu anaweza kufikia malengo yake na kuwa na maisha yenye furaha na mafanikio.

Haya sasa hapa hatuja kuonyesha ugumu tu wa kufanikiwa kama kijana au kukatisha ndoto zako za kufanikiwa angali kijana, tulichokifanya ni kukujuza tuu changamoto na nini kifanyike ili hata kama ukitaka kufanikiwa zaidi basi uwe uwezo wa kuepukana na changamoto hizo zinazowasumbua vijana wengi wa jinsia zote.

Usiache kufuatilia @Mwananchiscoop ili uweze kujua mambo mbalimbali kuhusiana na vijana, nasemajee tukutane tena next week halaaaaah!!!!.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags