Kijana anaefanana na Chris Brown kulipisha Tsh Milioni 3.5 kumuona

Kijana anaefanana na Chris Brown kulipisha Tsh Milioni 3.5 kumuona

Kumekuwa na tetesi kubwa mitandaoni ambapo media nyingi za nje ya nchi na hata hapa nchini zimeripoti kuwepo kwa kijana anayefanana na msanii wa miundo ya RnB na Pop, Chris Brown ambae anatoza dola 1500, sawa na Tsh milioni 3.5 za kiTanzania ili kuonana nae katika mji wa Detroit.

 

Kijana huyu anayejulikana kwa jina la Tyson Wuthi alianza kujizolea umaarufu baada ya kupost video kwenye mtandao wa TikTok ikionesha ni namna gani anafanana na msanii Chris Brown. Video hiyo inazaidi ya viewers milioni 1.



Hivi karibuni, ilizuka picha moja ambayo inaonesha msanii huyo akiwa ndani ya ndege, ambapo picha hiyo iliambatanishwa na maneno, "Going to be in Detroit this weekend, meet and greets $1,500″ written on top of it,” yaani atakuwepo katika nji wa Detroit wikiendi hii na kukutana na watu kwa dola 1500.



Hata hivyo, Wuthi alijitokeza na kukana tetesi hizo na kusema kuwa toka alipopata umaarufu kupitia video yake ya TikTok, watu wameanza kumzushia vitu vingi vya uongo kwani wataka achukiwe tu.

 
“THESE ARE ALL LIES ABOUT ME… I HAVEN’T MADE AN AGREEMENT WITH ANYONE,” he wrote on his Story. “I WOULD NEVER DO THAT… THE MEDIA LIES TO YOU JUST TO MAKE THE FANS GET MAD AT ME… DON’T BELIEVE IT,” aliandika Wuthi.



Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita tu, Chris Brown OG alifanya event yake ya "Meet and Greet" ambapo fans wake walilipia dola 1000, sawa na Tsh milioni 2.3 ili kupiga nae picha.... aise, iweje sasa Wuthi alipishe zaidi na yeye sio msanii?

Tuambie unafikiri huyu jamaa yuko serious ama anatest mitando tu? Tupia comment yako!






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags