Kifahamu kijiji kinachotumia jua bandia

Kifahamu kijiji kinachotumia jua bandia

Binadamu huwa wabunifu zaidi wanapopitia changamoto fulani, kauli hiyo unaweza kuielezea kutokana na ubunifu wa kulileta jua kwa kutumia kioo katika Kijiji cha Viganella nchini Italia.

Kijiji hicho kutokana na jiografia yake kuwa katika bonde lenye kina kirefu hukosa jua miezi mitatu mfululizo kwa mwaka, ili kukabiliana na jambo hilo mwaka 2006 wanakijiji waliamua kuchangishana fedha na kuweka kioo kikubwa chenye upana wa mita 8 na urefu mita 5 kwenye mlima mrefu uliopo katika eneo hilo.

Kioo hicho kipo umbali wa takriban mita 870 juu ya kijiji, kinadhibitiwa na kompyuta na kuakisi mwanga wa jua katikati ya kijiji, kikiuakisi kwa ufanisi.

Unaweza kuchangia nini ili kiweze kukusaidia wewe na majirani zako katika mtaa unaoishi?
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post