Khadija Kopa apewa tuzo ya mwanamke wa shoka

Khadija Kopa apewa tuzo ya mwanamke wa shoka

Mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania, Khadija Kopa amepewa tuzo ya Mwanamke wa Shoka kwenye sanaa yake ya muziki.

Tuzo hiyo alipatiwa kufuatiwa na kongamano la siku ya wanawake duniani linalofahamika kwa jina la “Kichen Party Gala,” iliyofanyika usiku wa kuamkia leo, katika ukumbi wa JC hall, Mbezi Beach.

Aidha, malkia huyo wa mipasho baada ya kupatiwa tuzo hiyo ya mwanamke wa shoka kwenye Sanaa ya muziki alitoa shukrani zake kwa kamati nzima.

Ikumbukwe tu, kwa zaidi ya miaka 10 ya uwepo wa tukio hili la kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Khadija Kopa amekuwa miongoni mwa waimbaji/waburudishaji kila mwaka.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post