KFC yafunga migahawa yake Lesotho

KFC yafunga migahawa yake Lesotho

Mgahawa maarufu ya vyakula vya haraka duniani KFC imelazimika kufunga matawi yote Lesotho baada ya kupiga marufuku bidhaa za kuku kutoka nchi jirani ya Afrika Kusini ambayo inakabiliwa na mlipuko wa homa ya mafua ya ndege.

Serikali kutoka Lesotho imepiga marufuku uagizaji wa kuku wote kutoka nchini humo, ambao KFC inasema umeathiri pakubwa usambazaji wake wa kuku, huku ikiwataka wateja wake kuwa wavumilivu hivyo itafunguliwa hivi karibuni.

Afrika Kusini imekuwa ikijitahidi kudhibiti homa ya mafua ya ndege kwa miezi kadhaa na imeua zaidi ya kuku milioni saba wanaotaga mayai.

Ikumbukwe tu Namibia pia ilipiga marufuku uagizaji wa kuku kutoka Afrika Kusini mwezi Septemba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post