Kesi ya unyanyasaji wa kingono yamkabili Foxx

Kesi ya unyanyasaji wa kingono yamkabili Foxx

Mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani anaye aitwaye Jane Doe anamtuhumu muigizaji na mchekeshaji James Fox kwa kumfanyia unyanyasaji wa kingono mwaka 2015.

Jane alidai kuwa Foxx alitumia silaha kumtishia kisha kumshika sehemu zake za siri huku akidai kuwa muigizaji huyo aliacha kumshika mara tuu baada ya rafiki wa mwanamke huyo kutokea.

Kwa mujibu wa Jarida la People limeeleza kuwa mwanamke huyo aliwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya juu jimbo la New York iliyoeleza kuwa kufuatiwa na tukio hilo lilisababisha Jane kupata majeraha na msongo wa mawazo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags