Kesi inayomkabili mwanamuziki wa bongo fleva Marioo na Meneja wake Sweetbert Mwinula iliyotakiwa kusikilizwa Machi 18 na 19, ya madai ya Sh550 milion imepigwa kalenda katika Mahakama Kuu Masijala ya Wilaya, Arusha hadi Mei 6, 2024.
Shauri hilo limesogezwa mbele kwa sababu ya kutokuwapo Mahakamani kwa Jaji Joachim Tiganga ambaye ndiye alitakiwa kusikiliza kesi hiyo pamoja na wadaiwa Marioo na Mwinula.
Licha ya hayo upande wa mdai kufika Mahakamani hapo lakini wadaiwa hawakufika
Ikumbukwe kuwa kampuni ya Kismaty ilimfungulia kesi mkali huyo wa Marioo na meneja wake kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza kwenye sherehe ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini iliyofanyika Septemba 23, 2021 .
Leave a Reply