Kesi ya Diddy yaendelea kupamba moto mahakamani

Kesi ya Diddy yaendelea kupamba moto mahakamani

Wakati mashahidi wakiendelea kutoa ushahidi kwa nyakati tofauti, timu ya wanasheria wa Diddy imeripotiwa kutaka kuondoa ushahidi wa Rapa Kid Cudi kwa madai ya kuwa ushahidi huo hauna mashiko yoyote.

Kwa mujibu wa TMZ, timu hiyo imewasilisha nyaraka kwa jaji inayoeleza kuwa Cudi anaamini Diddy huenda alihusika kuchoma gari yake aina ya Porsche mwaka 2021. Lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja wala ushahidi wa maandishi unaoonesha msanii huyo kuhusika huku wakiomba ushahidi huo utupiliwe mbali.

Utakumbuka kuwa wiki iliyopita rapa Cudi alitoa ushahidi mahakamani akidai kuwa Diddy alilipua gari yake kwa bomu aina ya Molotov baada ya kugundua kuwa Cudi ana mahusiano ya kimapenzi na Cassie Ventura.

Katika kesi hiyo aliyekuwa msaidizi wa Diddy, Capricorn Clark mapema leo anatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo akithibitisha kwamba alipokea barua pepe kutoka kwa Cassie pamoja na kuitwa na Cudi baada ya nyumba yake kuvamiwa.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa awali na Kid Cudi, ulieleza kuwa baada ya tukio la shambulizi la gari yake alimwita Clark na kumweleza tukio hilo. Lakini pia kutoa ushahidi kuhusiana na barua pepe iliyotumwa na Cassie mwaka 2011, ikieleza kuwa Diddy alikuwa akimtishia kusambaza video za ngono na kumdhuru yeye pamoja na Cudi.

Shahidi mwingine anayetarajiwa kutoa ushahidi leo ni pamoja na Maafisa kutoka Idara ya Polisi na Idara ya Zimamoto ya Los Angeles ambao watatoa ushahidi kuhusu matukio ya uvamizi na uchomaji moto wa gari la Kid Cudi mwaka 2012, ambayo yanahusishwa na Diddy.

Mpaka kufikia sasa zaidi ya mashahidi watano wameshatoa ushahidi kesi dhidi ya Diddy akiwemo aliyekuwa mpenzi wa rapa huyo Cassie Ventura, Mama wa Cassie Ventura, Dr. Dawn Hughes, Gerard Gannon. Huku msanii Kid Cudi akitarajiwa kutoa ushahidi kuhusu vitisho alivyopokea kutoka kwa Diddy baada ya kugundua uhusiano wake na Cassie.

Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York, baada ya kufunguliwa mashtaka ya shirikisho yanayohusisha njama ya kihalifu (RICO), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono kwa nguvu, udanganyifu au kulazimisha, na kusafirisha watu kwa ajili ya biashara ya ngono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags