Kesi ya Diddy na Cassie yafutwa mahakamani

Kesi ya Diddy na Cassie yafutwa mahakamani

Baada ya mwanamuziki na muigizaji kutoka nchini Marekani Cassie kufungua kesi mahakamani kwa madai ya kunyanyaswa kingono na mkali wa ‘rapa’ Diddy hatimaye kesi hiyo imefutwa mahakamani.

Hii inakuja baada ya wawili hao kufikia makubaliano ya kusuluhisha suala hilo kwa amani bila ya kutoa taarifa yoyote katika vyombo vya habari.

Cassie alifungua kesi mahakamani dhidi ya Diddy Novemba 16, mwaka huu akidai kuwa alibakwa, kuingizwa katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuhusishwa na biashara za kingono kwa zaidi ya miaka 10 walipokuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post