Kesi  ya Cardi B yafutwa

Kesi ya Cardi B yafutwa

Baada ya purukushani nyingi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kesi ya mwanamuziki Cardi B kumpiga shabiki na Microphone wakati akitumbuiza mjini Las Vegas wiki iliyopita, mwanamuziki huyo amefutiwa mashtaka hayo na hana ‘kesi’ tena.

Kwa mujibu wa TMZ news imeeleza kuwa wanasheria wa ‘rapa’ huyo akiwemo Drew Findling, David Chesnoff na Richard Schonfeld walipewa taarifa na idara ya ‘polisi’ mjini Las Vegas, kuwa kufuatia uchunguzi uliofanyika Cardi B hana shitaka la kujibu.

Ikumbukwe kuwa baada ya tukio hilo shabiki aliyepigwa na microphone hiyo alijitokeza na kumfungulia mashitaka Cardi B kwa alichomfanyia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags