Kenya yazindua mfumo wa kuwasilisha malalamiko mtandaoni

Kenya yazindua mfumo wa kuwasilisha malalamiko mtandaoni

Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kutoka nchini Kenya imezindua jukwaa la kidigitali ambapo wananchi wanaweza kuwasilisha malalamiko na kuomba ukaguzi wa kesi mtandaoni.

Jukwaa hilo linalojulikana kama Malalamishi system linawapa wananchi fursa ya kuwasilisha malalamiko ya jinai kwa odpp, kuwapa nafasi watoa taarifa (whistle blowers) na pia itarahisisha ufuatiliaji wa hali ya kesi kwani namba ya kumbukumbu itatolewa.

Vipi mwanetu jukwaa kama hili likizinduliwa kwetu Bongo utalitumia inavyopaswa? basi dondosha comment yako hapo tuone mtazamo wako katika hili.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post