Kendrick Lamar amejipata kwenye chati za Billboard

Kendrick Lamar amejipata kwenye chati za Billboard

Wakati bifu la wanamuziki kutoka Marekani Drake na Kendrick Lamar likiwa limepowa kwa muda, ‘rapa’ Lamar anaendelea kukimbiza na kuonesha ubabe katika chati za Billboard Hot 100 ambapo wimbo wake wa  ‘Not Like Us’ ukishika nafasi ya kwanza katika chati hizo.

Lamar aliuachia wimbo huo kwa ajili ya kumchana ‘rapa’ Drake ukiwa ni muendelezo wa bifu lao la kutoleana povu kupitia ngoma wanazo ziachia huku bifu hilo likiwa limefikia pabayo kutokana na watu watatu kukamatwa wakitaka kuvamia nyumba ya Drake ambapo mashabiki wanahusisha matukio hayo na bifu la wawili hao.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita Chati hizo za Billboard Hot 100, zilikuwa zikitawaliwa na bilionea na mwanamuziki wa Pop Taylor Swift ambapo nyimbo zake 10 zikiingia katika chati ya Billboard Top 10, ngoma hizo zikitoka katika album yake mpya ya ‘The Tortured Poets Department’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post