Kendrick Lamar adaiwa kuingia anga za Father John Misty

Kendrick Lamar adaiwa kuingia anga za Father John Misty

Rapa wa Marekani Kendrick Lamar anadaiwa kuingia kwenye anga za msanii Father John Misty, hii ni baada ya wawili hao kutoa album muda sawa kwa takribani miaka minne.

Utakumbuka kuwa jana Ijumaa Novemba 22, 2024 Lamar aliachia album yake aliyoipa jina la ‘GNX’ huku akiwashirikisha wasanii kama Jack Antonoff, Kamasi Washington, SZA na wengineo lakini kwa upande wa Misty naye alitoa album yake iitwayo ‘Mahashmashana’.

Kufuatia na Lamar kuachia album hiyo mwanamuziki Father John Misty aliingia katika mtandao wa twitter na kueleza kuwa hatomjibu msanii huyo sasa lakini anamvutia kasi ya kumjibu kupitia wimbo.

Hata hivyo kupitia posti hiyo mmoja wa shabiki alitoa maoni yake kwa kuandika kuwa Lamar amekuwa akifanya hivyo kwa miaka kadhaa nyuma ikiwemo mwaka 2012, 2015, 2017, 2022 na sasa 2024 huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa huwenda kuna jambo kati yao.

Na hizi ndio album walizozitoa katika miaka hiyo
2012: God Kid, M.A.A.D City (Lamar), Fear Fun (Father John Misty)
2015: To Pimp a Butterfly (Lamar), I love You Honeybear (Misty)
2017: Damn (Lamar), Pure Comedy (Misty)
2022: Mr Morales & the big steppers (Lamar), Chloe and the next 20th century (Misty)
2024: GNX (Lamar), Mahashmashana (Misty)






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags