Kehlani adai kukosa ‘madili’ kisa Palestina

Kehlani adai kukosa ‘madili’ kisa Palestina

Mwanamuziki kutoka Marekani, Ashley Parrish, ‘Kehlani’, ameweka wazi kuwa alipata hasara kwa kupoteza fursa za mikataba baada ya kutoa msaada kwa watu wa Palestina.

Kehlani ameyasema hayo siku ya jaan Jumanne Juni 25 kwenye mahojiano yake na ‘Breakfast Club’ akidai kuwa amerudi nyuma kimaisha kwa kupata hasara lakini hajutii kufanya hivyo.

“Nimepata hasara nyingi na kupoteza vitu vingi ambayo niliahidiwa kama uchapishaji wa albamu na fursa nyengine katika muziki” amesema.

Hata hivyo msanii huyo ameeleza kuwa hajutii kufanya jambo hilo kwani sasa anaweza kulala kwa Amani huku akijua kwamba kuna watu walipata msaada kupitia yeye.

Mei 29 mwaka huu Kehlani aliwaunga mkono watu wa Palestina kupitia ukurasa wake wa  Instagram kwa kuonesha video iliyo kuwa na bendela ya Palestina, hivyo basi kupitia post ya Kehlani zilipatikana Dola 500,000 ambazo zilikusanywa kwa ajili ya watu wa Gaza, Kongo na Sudan.

Kehlani mwenye umri wa miaka 29 amewahi kufanya ngoma kama ‘Good Thing’, ‘I Lake That’, ‘After Hours’, ‘Toxic’, ‘Good Life’, ‘Night Like This’, ‘Gangsta’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags