Katompa Atua  Songea

Katompa Atua Songea

Ebwana eeeh, tayari Bondia Mkongoman Erick Tshimanga Katompa amewasili Songea Kwa ajili ya  Pambano lake dhidi ya Seleman kidunda Litakalo pigwa Julai 30, Mwaka huu katika uwanja wa Maji Maji.

Akizungumza Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Songea Airport Amesema Yupo Tayari kwa Pambano hilo na niheshima kubwa kwa Rais Wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan Kwa mapokezi mazuri aliyoyapata hivyo wanasongea na Watanzania wasubiri burudani ya aina yake usiku huo.

 Kwa Upande wake kocha wa bondia huyo Junior Asoya, Amesema wamekuja Tanzania kuchukua mkanda wao Wa WBF.

Hata hivyo Promota wa Pambano hilo ambaye ndiyo waandaaji Kutoka PeakTime Meja Seleman Semunyu Amesema Hii ni ishara Kuwa Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90 kinachosubiriwa ni siku ya kushuhudia Pambano hilo kubwa la kimataifa la PayBack Night.

Nikukumbushe tu kuwa Pambano hilo Litakalo Kutanisha miamba miwili ya Ngumi kati ya bonda Seleman kidunda na Mkongo man Erick Tshimanga Katompa wakiwania Ubingwa wa mkanda wa WBF Julai 30,mwaka huu katika uwanja wa majimaji songea Mkoani Ruvuma.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags