Katazo wanamichezo wanawake kuvaa hijabu lazua mijadala

Katazo wanamichezo wanawake kuvaa hijabu lazua mijadala

Ikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa, uamuzi wa nchi hiyo kuzuia wanawake kuvaa hijabu katika michuano umezua mijadala na upinzani kutoka kwa makundi ya haki za binadamu na kwa wanajamii, kwa madai ya kuwa ni kuvunja uhuru wa kidini na haki za kibinadamu.

Katazo hilo lilitolewa tangu mwezi Septemba, 2023. Likilenga kuzuia wanawake Waislamu kuvaa hijabu au aina nyingine za mavazi ya kidini wanaposhiriki katika michezo, kama vile mpira wa kikapu, soka na volebo.

Kutokana na hayo Ufaransa imefafanua kuwa marufuku hiyo inawahusu wanamichezo wanaoshiriki mashindano ndani ya nchi, na siyo kutoka mataifa mengine.

Aidha kwa upande wa Umoja wa Mataifa, wameeleza kuwa hakuna mtu anayepaswa kumpangia mwanamke avae au asivae kwa mujibu wa imani yake. Hivyo Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa uhuru wa kujieleza kuhusu dini au imani, ikiwemo chaguo la mavazi, ni haki ya msingi ya kila mtu.

Ikumbukwe kuwa michuano hiyo inatarajia kuanza Jul 26 hadi Aug 11 mwaka huu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags