Karen na mashabiki kuwaombea akina mama

Karen na mashabiki kuwaombea akina mama

Msanii wa muziki wa #BongoFleva @malkiakaren, ameonesha shukurani zake kwa akina mama wote wanaosali kwaajili ya familia zao.

Malkia ambaye pia kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja, ameamua kuungana na mashabiki wake, katika mtandao wa #Instagram kuwaombea akina mama hao wenye tabia ya kusali saa tisa za usiku kwaajili ya familia zao.

Mrembo huyo aliwataka wafuasi wake wa #Instagram ku-comment amen katika post aliyoandika, “Asante Mungu kwa mama wanaosali saa tisa za usiku kwa ajili ya familia zao”.

Jambo hilo limepelekea kuamsha hisia za baadhi ya mashabiki, kwa kila mmoja kueleza ambavyo mama yake anapambana kusali kwa ajili ya familia, huku wengine wakiendelea ku-comment amen katika post hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags