Karani wa Sensa Ajinyonga

Karani wa Sensa Ajinyonga

Wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likiendelea huko mkoani Tabora Karani wa sense ya watu na makazi aliyetambulika kwa majina  Edimundi Zakayo amejinyonga.

Akithibitisha kifo cha karani huyo  Mkuu wa mkoa wa Tabora, Balozi Dkt Batilda Buriani, ameeleza kuhusu tukio la mwalimu mmoja kujinyonga aliyejulikana kwa jina la Edimundi Zakayo kutoka wilaya ya Igunga ambaye alikuwa ameajiriwa na serikali katika zoezi la uhesabuji wa watu na makazi mkoani humo.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwamba, chanzo cha kifo cha Karani huyo ni matatizo ya kifamilia na kwamba kabla ya kujiua, aliandika barua ambayo ilielezea mambo mblimbali ikiwemo chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo wa kujiua.

Hata hivyo , hakuna kifaa chochote kilichoibiwa wala kuharibika na hivyo vifaa hivyo vilichukuliwa na kupewa mtu mwingine ambaye anaendelea na zoezi hilo la kuhesabu watu huku viongozi wakiendelea na taratibu mbalimbali za kuweza kumpumzisha ndugu Edimund Zakayo katika nyumba yake ya milele






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags