Kanye West na Kim Kardashian wadaiwa kurudiana

Kanye West na Kim Kardashian wadaiwa kurudiana

Katika hali isiyo ya kawaida Rapa kutokea nchini Marekani Kanye West na mzazi mwenzake Kim Kardashian unambiwa ni kama wamevuka mipaka ya urafiki wao na uwenda kama wamerudiana.

Unaambiwa licha ya kuwa na utaratibu wa malezi wa pande zote mbili kwa watoto wao wanne yani kushirikiana na Kim kuwalea pamoja, wawili hao wameonekana wakitoka pamoja huko Malibu na watoto wao wote wanne baada ya kupata chakula cha usiku.

Hayo yote yameibua maswali kutoka kwa mashabiki wao na wengi wanasema uwenda wawili hao wamerudiana kimapenzi kwani sio mara ya kwanza kuonekana pamoja katika mtoko wa kimahaba zaidi.

Itakumbukwa hata usiku wa Listening Party ya 2 (Donda Album), Kim alionekana akiwa amevalia vazi la harusi suala ambalo wengi walibaki kujiuliza bila kupata majibu.

Je msomaji wetu kwa ukaribu wa wawili hawa ni kweli wamerudiana au wanatuzuga, dondosha comment yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags