Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.
Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani.
Zifuatazo ni Kanuni na Mbinu mhimu za kuishi na watu vizuri.
1: Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote, hali kadhalika na wewe watakupenda.
2: Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana.
3: Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake,hata akiwa ni masikini ,hakuelimika,hana cheo cha juu na kadhalika.
4: Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu.
5: Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe.
6: Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga.
7: Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya.
8: Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu.
9: Shukru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante au shukru kwa kila jambo.
10: Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa.
11: Usipende mabishano na kama yakitokea,usitake kila mara kushinda.
12: Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu.
13: Usipende kugombana,kupiga au kupigana na watu.
14: Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu.
15: Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki.
16: Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea.
17: Usiwe unachonganisha watu,ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesema.
18: Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo.
19: Tunza siri zako na za wengine.
20: Usiwe mwepesi wa hasira
21: Kumbuka majina ya watu unaokutana nao.
22: Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri.
23: Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli.
24: Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda.
25: Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika.
26: Jifunze kusamehe makosa ya watu.
27: Unapofanya makosa, kubali na kuungama na kuomba msamaha.
28: Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako.
29: Nigongee like hata kama hujaipenda hii.
Leave a Reply