Kane hashikiki Ulaya

Kane hashikiki Ulaya

Baada ya watu wengi kuona pengine asingekuwa na makali baada ya kujiunga na ‘klabu’ ya #BayernMunich akitokea katika ‘klabu’ ya #Tottenham, #HarryKane amezidi kuwa mtamu.

Kane amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Munich akiwa amecheza ‘mechi’ 16 za michuano yote na kufunga mabao 21.

Kwa upande wa #Bundesliga yeye ndiye kinara wa utupiaji akiwa amefunga mabao 17 kwenye ‘mechi’ 11.

Pia kwenye ‘timu’ ya taifa katika ‘mechi’ mbili za mwisho za kuwania kufuzu Euro 2024, ameweka kambani mabao matatu, mawili akifunga dhidi ya #Italia kwenye ushindi wa mabao 3-1 na moja akafunga dhidi ya ‘klabu’ ya #Malta.

Kiwango chake akiwa katika ‘timu’ ya England kimeisaidia taifa hilo kufuzu mapema Euro kabla hata ‘mechi’ za makundi hazijamalizika ikiwa imecheza ‘mechi’ saba ikishinda sita, sare moja, kwenye‘mechi’ hizo saba Kane amefunga jumla ya mabao saba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post