Kampuni ya Johnson & Johnson yashtakiwa Kenya

Kampuni ya Johnson & Johnson yashtakiwa Kenya

Shirika moja la kutetea haki za binadamu kutoka nchini Kenya limeishtaki shirika la kimataifa la Marekani Johnson & Johnson juu ya kuuzia wananchi wao poda zisizo na ubora.

Shirika la African Centre for Corrective and Preventive Action limesema kuwa ingawa bidhaa hiyo ilipigwa marufuku katika nchi kadhaa kama vile za Bara Ulaya na India bado inauzwa nchini Kenya.

Katika ombi lililowasilishwa lenye kuangazia kulinda haki ya mnunuzi, shirika hilo linadai kuwa kampuni ya Johnson & Johnson linatumia benzene na talc kwenye bidhaa zake za poda ya watoto.

Aidha shirika hilo linadai kuwa benzene na talc inasababisha saratani kwa binadamu na kuwa talc yenye madini ya asbesto husababisha madhara makubwa kwa mtumiaji wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags