Kambole sababu ya Yanga kufungiwa kusajili

Kambole sababu ya Yanga kufungiwa kusajili

Shirikisho la la mpira wa miguu (FIFA) limeifungia ‘klabu’ #YangaSc kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Lazarus Kambole baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Taarifa ya shirikisho la soka la mpira Tanzania (TFF) imebainisha kuwa Kambole raia wa Zambia alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba.

“Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.” imesema taarifa ya TFF.

Hivyo TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags