Kabla ya Mondi na Wema alikuwepo Nature na Sintah

Kabla ya Mondi na Wema alikuwepo Nature na Sintah

Juma Kassim Kiroboto. Hata spika za studio, redioni na jukwaani zilinyenyekea sauti na viitikio vyake. Kibra Matata 'Saa Necha' katika wakati wake. Aibu!

Ni yeye aliyefanya Manyema Family ya Chegge ifike mjini kwa kiitikio tu. Ni yeye aliyemfanya Mike Tee atoroke sana chuo. Shoo zilipoongezeka baada ya kiitikio cha ngoma ya 'Nampenda'.

Mkono wa P Funk na koo la Nature. Huu ni muunganiko bora kuwahi kutokea, ni kama kitunguu na nyanya. Walipojifungia studio pale mitaa ya Bamaga, walitoa 'mabomu' yaliyofanya tusahau shida zetu.

Alibadili 'laifu' ya washikaji kibao mitaani kwa zawadi ya kiitikio tu kwenye simbo. Leo hii anaweza kufanya shoo ya 'korasi' zake tu watu wakadata. Siyo bahati mbaya haya kutokea, kuna kazi kubwa ilifanyika.

Nipo Gado ya Zay B, Mtani Jirani ya Joint Mobb, Mtulize ya Mabaga, Zali la Mentali ya Prof. Jay. Ni pini zilizopambwa viitikio vyake kwa sauti Kuna Nature. Muziki wa Tembele ulikuwa begani kwake.

Nature pamoja na umaarufu wake katika muziki. Lakini umaarufu uliongezeka zaidi baada ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na Sintah. Uhusiano wao uliandikwa na kuongelewa sana mitaani.

Lilikuwa 'kapo' moja bab kubwa. Mtoto wa uswahilini anakamatia 'pisi kali'. Ni kama walikuwa na dunia yao ndani ya dunia hii. Na baada ya kutemana bado waliendelea kuwa midomoni mwa watu.

Nature na Sintah ni kama Mondi na Wema kipindi kile. Na inawezekana ya Nature na Sintah yalikuwa juu zaidi. Pata picha ingekuwaje katika dunia ya sasa ya mtandaoni. Wao walitamba kurasa za magazeti.

Hakuna shoo kubwa iliyofanyika hapa Dar es Salaam bila Juma Nature. Muziki ulikuwa ni Nature na Nature alikuwa ni muziki kamili. Tmk Wanaume Family ni moja ya nguzo muhimu katika maisha yake.

Kuna ndoa tamu ilifungwa kati yake na P. Funk Majani. Alikuwa msanii pendwa wa Bongo Records. Studio ilizunguka kupitia Juma Nature. Ukataka jambo lako kwa Majani, ilikuwa rahisi zaidi ukimtumia Kibra.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags