Jux afunguka ujauzito wa Vanessa

Jux afunguka ujauzito wa Vanessa

Leo huko mitandaoni kimeumana, unaambiwa mwanamuziki nchini Tanzania, Juma Mkambala maarufu kama Jux ametoa nyimbo na kumpatia hongera aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee kwa kupata ujauzito.

Jux ametoa hongera hizo baada ya kusambaa kwa picha za Vanessa zikimuonesha kuwa mjamzito na kuweka wazi kuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume siku za hivi karibuni.

Hata hivyo katika ukurasa wake wa Instagram msanii huyo aliandika ujumbe mahususi kwenda kwa Ex wake huyo ikiwa ni baada tu ya kuachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la “Sina Neno na siku moja kupita baada ya Vanessa kuitangazia dunia kuwa ni mjamzito.

Kupitia ukurasa huo, Jux amesema hata kama mambo hayakuenda sawa kama ambavyo alipanga hana sababu ya kumchukia mtu maana aliagizwa upendo.

“Tuliagizwa upendo, Hata kama mambo hayakwenda kama ambavyo mlipanga, hauna sababu ya kumchukia wala kumuombea mtu yeyote mabaya, zaidi kwenye jambo jema lenye Baraka.

“Ukielewa kuwa sio mara zote kitu kizuri kinadumu, hakuna changamoto yoyote itakayokusumbua, let’s enjoy some good music #sinaneno,” aliandika Jux

Hata hivyo katika wimbo wake huo mpya, King Of Hearts amemtakia kheri na kumuombea maisha mema na yenye furaha baada ya kuiona familia ikikuwa.

Moja ya line kutoka kwenye wimbo huo inasema “Tushafunika kurasa mambo ya zamani yalishapita, maisha mengine sasa kuwa na amani hakuna vita, sikuchukii nakuombea maisha mema na ya furaha, Mungu aonyeshe njia”

 






Comments 1


  • Awesome Image
    Metey

    nikweli maisha yaendelee tu bifu sjui kuwek jamb moyon kunarudish maendeleo nyum wakat wakumtafakar mtu ama kitu fulan huo ndio mud ambao unatakiw kufany marekebish yakile kilichoend sivyo si kwa lawama Bal kujikwamua kifikwa na kimatend hap maish yatakuw yanaendelea lasivyo ukidil na uhasam yakwamb ilikuw hivi ikawa vile maish hayaend Bali yatakuw hap t nikumtumainia mwenyez mung na kuamin yakwamb Kila jamb huja kwa sababu hutokea na kuondok pia nikwa sababu fulan"

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags