Jumatano Usher hali chakula chochote

Jumatano Usher hali chakula chochote

Mwanamuziki kutoka Marekani Usher Raymond ameweka wazi kuwa kila ifikapo siku ya Jumatano huwa hali chakula chochote zaidi ya kunywa maji.

Usher ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na jarida la WSJ ambapo alitoa sababu ya kufanya hivyo ni kuendeleza alichokuwa akikifanya marehemu bibi yake ambapo amekuwa akifunga kwa mwaka sasa.

“Mimi hufunga, si kwa madhumuni ya kidini, lakini ni jambo ambalo bibi yangu alizoea, Kwa kawaida mimi hujaribu kuanza karibu saa 11 jioni Jumanne na siku nzima Jumatano huwa nakunywa maji tu”

Mshindi huyo wa Grammy mwenye umri wa miaka 45 ameyasema hayo wakati alipokuwa akieleza kuhusiana na ratiba zake za mlo pamoja na mazoezi ambapo alidai kuwa huwa hapendi kabisa kunywa kifungua kinywa kabla ya mazoezi.

“Sipendi kula kiamsha kinywa kabla sijafanya mazoezi au kufanya jambo fulani la kimwili kama kutembea, kujinyoosha au kufanya yoga, kuketi kwenye jua na kunyoosha viungo vyangu nikimaliza ndio naweza kula” amesema Usher.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags