Jose Chameleon arejea mzigoni

Jose Chameleon arejea mzigoni

Baada ya kupata matatizo ya Ini na Kongosho hadi kupelekea kulazwa hospitalini, nguli wa muziki kutokea nchini Uganda, Jose Chameleone (42) amedokeza ujio wa wimbo wake wa kwanza 'Forever' baada ya kupona.

Wimbo huo amepanga kuutoa Oktoba 9, mwaka huu ambapo itakuwa siku ya Uhuru nchini Uganda huku ukiwa umetayarishwa na Ian Pro na Yaled.

Itakumbukwa kuwa Agosti 23, 2021 Staa huyo  mkubwa wa muziki barani Afrika aliripotiwa kulazwa hospitalini kwa tatizo la Ini na Kongosho.

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari nchini Uganda ilieleza kuwa Chameleone amelazwa kwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda kidogo.

Hivyo ni jambo jema kusikia nguli huyo anarejea tena mzigoni baada ya kupona...






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags