Johari: siwezi ku-force ndoa

Johari: siwezi ku-force ndoa

Star mkongwe wa filamu nchini, Johari Chagula amefunguka na kusema kuwa hawezi kuforce kuolewa ila anaimani kuwa wakati wa sahihi wa Mungu utafika na ataolewa.

Maneno hayo ya Johari yametrend katika mitandao huku baadhi ya mashabiki zake wakihoji uwenda amekuwa akichagua sana wanaume jambo ambalo ndilo linamkwamisha kuolewa mpaka sasa.

Hata hivyo mwanadada huyo amefunguka na kusema kuwa, kila kitu ni mipango ya Mungu na hawezi ku-force ndoa kama watu wengine wanvayofanya.

“Unakuta watu wengi wana-force mahusiano au ndoa mwisho wa siku anaachwa na wakati mwingine kufanya vitu ambavyo vinaweza kukutoa utu wako.

“Kwa hiyo mimi kama mimi siwezi kuforce ndoa, siwezi kumnganganiza mtu anioe, nasubiri wakati sahihi wa Mungu, najua utafika wakati wangu na mimi nitaolewa, sidhani kama ndoa ina mwisho hata uwe na miaka mingapi ikifikia kuolewa utaolewa tu,” alisema

Alisema maneno ya watu hayawezi kumuumiza kwa sababu hata angeolewa akiwa na umri wa miaka 20 au 18 ingeweza kumshinda hivyo anavuta subiria na itakapofikia muda wake ataolewa.

Aidha Johari alisema yeye ni mkubwa lakini kutokana na maisha ya Tanzania amekuwa akionekana kama mdogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags