Johannesburg  mafuriko yauwa watu 9

Johannesburg mafuriko yauwa watu 9

Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa nchini Afrika Kusini yamesababisha vifo vya watu tisa(9) waliokuwa wakishiriki ibada za kidini mjini Johannesburg.

Kitengo cha kukabiliana na majanga nchini humo kimesema kundi la waumini 33 walikuwa wamekusanyika kanisani katika eneo la ukingo la mto Jukskei kabla ya tukio hilo.

Aidha vikosi vya waokozi na zima moto bado vinaendelea na jitihada ya kusaka miili ambayo haijapatikana mpaka sasa, Mikasa ya ghafla ya kuongezeka kwa maji ni ya kawaida katika sehemu hiyo ya Johannesburg, ambapo dhoruba hutokea karibu kila usiku wakati wa majira ya joto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags