Joh Makini amvaa Sallam Sk Twitter, warushiana maneno

Joh Makini amvaa Sallam Sk Twitter, warushiana maneno

Hivi unaikumbuka Don't Bother ya Joh Makini ft AKA? unaambiwa wimbo huo umezua maneno huko Twitter baada ya Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam SK kusema ameunganisha ngoma hiyo kufanyika bila malipo yoyote.

Joh Makini aka-comment kwenye post hiyo kwa kusema Sallam aelezee ameiunganisha vipi kwani alipambana sana kukwamisha wimbo huo usifanyike.

"Aelezee aliunganisha vipi yeye sio chanzo cha hiyo collabo, kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki wa Pili na G NakoWarawara lakini waliomleta walikua hawataki itokee".

"Muarabu alipambana sana kukwamisha hii basi tu Mwenyezi Mungu hajawahi kushindwa" ameandika Joh Makini

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags