Jinsi ya kuwa na muonekano mzuri siku ya mahafali (graduation) yako

Jinsi ya kuwa na muonekano mzuri siku ya mahafali (graduation) yako

Naam!! tunakutana tena kwenye ulimwengu wa mambo ya fashion na urembo, I hope mko poa watu wangu wa nguvu tunaendelea tulipoishia katika kapu letu hili la fashion katika magazine yetu pendwa ya Mwananchi Scoop.

This weekend katika fashion tutazingatia muonekano mzuri na namna ya kuvaa siku ya graduation, sasa hapa wanafunzi wenzangu tujuane katika mada hii.

Ili kupata muonekano huo wa kipekee haswa kwa wahitimu wa vyuo vikuu wanapaswa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo uvaaji wa nguo' classic' zinazoendana na tukio lenyewe, uvaaji wa viatu rasmi vitakavyokufanya kuwa huru pamoja na upakaji wa make-up ya wastani kwa wahitimu wa kike hapa kwenye make-up ni kwa wale wanaopenda muonekano huo.

Akizungumza na jarida la Mwananchi Scoop mtaalamu wa masuala ya urembo Aisha Mtawa anaeleza kuwa mahafali ni moja kati ya siku muhimu sana kwa mwanafunzi katika maisha yake ya kielimu hivyo ni muhimu aonekane classic kuliko siku zote.

Mwanadada huyo alisema mahafali ni sherehe lakini ipo katika mfumo rasmi hivyo ni vyema kuvaa nguo rasmi lakini zilizo classic na zenye mitindo ambayo itakufanya kutoka kitofauti anaseama.

"Zile nguo zetu za kumeremeta za kwenye harusi na sendoff, kwenye sherehe za mahafali siyo mahala pake,"

Pia ameshauri kwa wahitimu wa kike kujiepusha na uvaaji wa nguo fupi na zenye kubana sana kwani zinaweza kuwafanya kushindwa kuwa huru kusherehekea si unajua siku hiyo lazima kuwe na wageni rasmi kwa hiyo haifai kuvaa nguo zisizo kuwa na heshima.

Anaendelea kutueleza mwanadada Aisha "Ili kupata mavazi yatakayokupa muonekano mzuri ni vyema kufanya maandalizi mapema na kufanya utafiti ni wapi utapata nguo nzuri au mbunifu wa mavazi atakayeweza kukushonea nguo itakayokupa muonekano mzuri katika siku hiyo muhimu"

Kwa upande wa viatu Aisha alisema uvaaji wa viatu mara nyingi huendana na tukio linalofanyika katika eneo husika hivyo kwa kuwa shughuli hiyo ni rasmi hivyo inapendeza zaidi wahitimu wa kike na kiume kuvaa viatu vilivyo rasmi na vitakavyowafanya kuwa huru zaidi.

"Piga picha mwanaume kavaa suti nzuri then chini akavaa sendo au ndala hii itaharibu mvuto wake  kutokana na kutokuwa na muunganiko kati ya nguo na aina ya viatu alivyovaa,"alisema.

Vilevile aliwataka wahitimu wa kike kuacha tabia ya kuiga kuvaa viatu virefu sana ambavyo hawana uwezo wa kutembea navyo hali inayowapa changamoto katika kutembea.

Katika upande wa masuala ya make-up na nywele  kwa wahitimu wa kike mtaalamu mwingine wa masuala ya urembo Jackline George alisema ni vyema wahitimu hao kujiepusha na usukaji wa nywele au ‘rasta’ zenye rangi rangi kwani linaweza kuleta tafsiri tofauti kwa kuwa tukio hilo ni rasmi anasema.

"Tukio hilo ni rasmi hivyo usukaji wa nywele za rangi rangi au unyoaji wa mitindo isiyokuwa rasmi inaweza kuleta tafsiri isiyo nzuri kwa wageni waalikwa.

Kwa upande wa makeup kwa wahitimu wa kike Jackline alisema ni muhimu kwani inafanya muonekano wake kuvutia zaidi na ni vyema kupaka simple make-up ambayo inadumu kwa muda mrefu.

Hapa sasa nitakushangaa Mwananchi Scoop imekuelekeza namna utakavyotoka siku yako ya Graduation wewe mwanachuo kisha mambo yakaenda hovyo na ndiyo maana lazima tukwambie ili uwe naamani unapotaka kutoka kifashion.

Labda tu mimi nikwambie hayajaisha mpaka yaishe watu wangu wa nguvu nikimaanisha mwisho wa mada hii this week kwenye fashion ndiyo mwanzo wa mada nyengine next week katika kapu letu hili hili la fashion. Usibanduge kila weekend katika Magazine ya Mwananchi Scoop.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags