Jinsi ya kuwa na muonekano mzuri katika vazi la sherehe

Jinsi ya kuwa na muonekano mzuri katika vazi la sherehe

Alooo weeeee!! Guyz natumai ni wazima wa afya, kama kawaida yetu hatunaga mba mba mba yaani moja kati ya vitu ambavyo najua/naamini kila mtu anapenda kuwa na muonekano mzuri  sidhani kama kuna mtu atapingana na mimi.

Leo katika kapu letu la fashion nikusogezee kitu ambacho this weekend utajifunza kitu mwanetu, hivi unajua fashion ina bebwa na muonekano wa mtu kimavazi, basi team scoop ina mengi sana ila leo ngoja tuzungumzie kwanza muonekano katika mavazi ya sherehe.

Moja kati ya jambo linaloshauriwa na wataalamu wa mitindo katika kutengeneza muonekano wa kuvutia ni pamoja na uvaaji wa nguo inayoendana na mwili yaani inayokutosha vizuri bila kukubana.

Muonekano ni pamoja na kufanya fitting hii inahusisha marekebisho ya mwisho yanayofanyika katika nguo ikiwa ni pamoja na urefu na upana pamoja na marekebisho mengineyo kabla ya kuvaliwa kwa nguo ili kuifanya iendane na muonekano wa mwili kwa wakati huo.

Hivyo inashauriwa kufanya fittings ya nguo unayotarajia kuvaa katika shughuli siku chache kabla ya siku hiyo kufika unapovaa nguo yako iweze kuendana na mwili wako jambo litakalosaidia kupendezesha muonekano wako.

Hapa sasa team ya Mwananchi Scoop ilimfikia kwa Abdul Kilumbi ambaye ni fundi wa nguo za sherehe kutoka Kilumbi Fashion anaeleza kuwa vazi lililoshona na na kubuniwa vizuri humfanya mtu kupendeza lakini inapokutosha vyema huboresha zaidi muonekano wako na kukufanya kuwa huru kutembea na hata kucheza pia.

Alisema ili kupata muonekano huo ni vyema kufanya fitting kwani kuna mabadiliko mbalimbali ya mwili huweza kutokea mfano kunenepa au kukonda sana hivyo kupitia fitting utapata muonekano wa nguo unayoendana na mwili kwa wakati huo.

"Miili yetu huwa inabadilika mfano kwa upande wa bibi harusi anaweza akawa ameshona nguo yake miezi miwili kabla ya shughuli akiwa amenenepa lakini kutokana na hekaheka za shughuli anaweza akapungua kiasi hivyo atakapovaa nguo yake bila kuifanyia marekebisho ya kuifanya iweze kuendana na mwili inaweza kuharibu muonekano wake katika siku yake hiyo muhimu,"alisema.

Hivyo ni vyema siku tano hadi tatu kabla ya tarehe ya shughuli kuonana na fundi aliyekubunia na kushonea nguo yako kwa ajili ya kufanya marekebisho hayo.

Alisema kuwa marekebisho hayo si kwa ajili ya nguo za sherehe pekee lakini pia inashauriwa hata kwa nguo ulizoshona kwa ajili ya kuvaa maeneo mengine kama vile ofisini yanapaswa pia kufanyiwa marekebisho hayo anasema.

"Lakini pia marekebisho hayo yanaweza kufanywa hata kwa nguo ambayo umeinunua dukani na kutokutosha vyema kwa kumuona fundi cherehani ambaye atakushauri nini kinachopaswa kufanyika kulingana na muonekano wako,"alieleza Abdul

Vilevile aligusia swala la wanaume kuwa nyuma katika ufanyaji wa fittings pindi wanaposhona nguo zao akitolea uzoefu wake wa miaka saba katika kazi ya ushonaji nguo anaeleza.

"Kwa uzoefu wangu Mara nyingi wanawake ndio wamekuwa wakizingatia sana swala la ufanyaji wa fittings wanaposhona au kununua nguo zao ukilinganisha na wanaume,"alisema fundi huyo

Alisema ni vyema na wao kuzingatia jambo hilo kwani wanapovaa suti au aina nyingine za nguo zinazowatosha vizuri kulingana na muonekano wao huzidi kuboresha utanashati wao

"Kuvaa nguo inayokutosha vizuri na kuendana na mwili wako ni muhimu kwani mara tu unapokutana na mtu anapata tafsiri mbalimbali kuhusu wewe kutokana na muonekano wako, ukionekana na mavazi makubwa au madogo kuliko wewe humpa tafsiri tofauti ikiwemo kuwa hujali muonekano wako”alisema Abduli

Hatukishia hapo tulifika hadi mkoa wa pwani tukakuta na mwana mama Mwanaheri Hamadi yeye nifundi wa kushona nguo za kike nyumbani kwake hapo.

Alieleza yeye kwa upande wake anasema hakubali kumpa mteja wake nguo mpaka afanye fitting tena hapo anaweza akakosana na mteja kwa sababu yakujishushia cv yake kama navyoeleza.

“Mimi huwaga sipendi kabisa mteja anapo acha kuja kujaribu nguo yake ili aweze kuona kama imemkaa mwili, sababu mteja nguo yake itakapo mkaa vizuri lazima na mimi ntapata wateja huwa na washauri tu wateja wangu wanakuja kujaribisha nguo kabla sjafanya finishing”alisema mwanaheri.

Ingawa nakuwa namisimamo hiyo kwa wateja wake lakini bado imekuwa changamoto ya kutofanya fitting yanguo kwa wateja wake mpaka kuna time inampa ugumu na malalamiko yanakuja kwake kuwa ameshona vibaya

 “Watu wanapenda kuona matokeo chanya kwenye mionekano wakiamini mafundi ndio wanaharibu sasa mtu anambia aje kufanaya fitting ya nguo yangu anakupa singizio yuko bize”alisema mama huyo

Acha tu niwaambie fashion ina vitu vya kuzingatia waweza ukamuona mwenzako amependeza kutokana muonekano wake mwenzio alizingatia mpaka hilo vazi lake kuwa na muonekana sasa wewe una kurupuka utaki kufanya fitting ya vazi lako muonekanao mzuri utauona wapi? Lazima utoe boko hapo sisi team Scoop tushakueleza kazi ni kwako mwanetu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post