Na Aisha Lungato
Ni matumaini yangu wazima wa afya, so tunandelea pale tulipoishia siku hizi waswahili tunasema hakuna kupumzuka, mpaka watuite matajiri, leo katika biashara tumekuja na biashara ambayo anaweza akaifanya mtu yeyote, kwa sababu unaweza kuifanya kwa muda wako wa ziada hata kama una majukumu mengine.
Kwenye baadhi ya nyumba Bongo katika kila mlo wao lazima kuwe na kichangamsha mdomo, yaani pilipili, ambapo bila kitu hicho wengine wanaweza wasione chakula kama kinaladha kabisa, na kama ukiona mtu hali pilipili basi labda anaweza kuwa na vidonda vya tumbo.
Sisi wazee wa kuona fursa tumekuja tena na fursa hii nyingine ni wewe kuchagua kulala nyumbani au ujishughulishe ili uweze kupata pesa za ku-solve matatizo yako, tuzungumze yote lakini biashara ya pilipili siku hizi imekuwa ikishamiri siku hadi siku kutokana na watu kuzipenda.
Bei zake kwa chupa huanzia tsh1000 hadi tsh5000 vipi ukiuza chupa zako kumi kwa siku? utakuwa wapi, so ili uweze kutoboa katika biashara hii inabidi kwanza ukubali kuzunguka.
Kwa sababu biashara hii inahitaji mtu mchangamfu haswaa, na mara nyingi biashara hii hufanyika, kwenye masoko ya vitu mbalimbali, unaweza kwenda kuomba kuweka katika duka lililopo karibu yako na hata kwenye magenge pia.
Mahitaji
- Unaweza kuanza na karoti sado 1, au hata kilo moja
- Pilipili kumi 20-40 (kama unataka iwashe sana)
- Nyanya 10 (zilizoiva vizuri)
- Vitunguu maji na swaumu kiasi ( hata 5)
- Tangawizi 5
- Chumvi
- Vinegar chupa tatu hadi 4
- Solium benzoate kijoko kimoja
- Mafuta ya kula lita/ nusu lita
JINSI YA KUTENGENEZA
Osha karoti zako vizuri, siyo lazima uzimenye kisha zikatekate.
Ondoa vikonyo kwenye pilipili zako, kisha katakata nyanya, vitunguu maji, na swaumu kisha weka vyote kwenye sufuria zikiwemo karoti zako.
Tia chumvi, mafuta ya kula na vinegar chupa moja kisha weka jikoni na uache vichemke wa dakika 15-20.
Epua acha pilipili yako ipoe kidogo kisha mimina mchanganyiko wako katika blender na usage pilipili yako.
Unaposaga pilipili yako hutakiwi kutumia maji bali utatumia vinegar kusagia pilipili yako.
Baada ya pilipili kusagika vizuri chukua ‘Solium benzoate’ kijiko kimoja au viwili changanya na ukoroge.
Na mpaka kufikia hapo pilipili yako itakuwa tayari , andaa chupa zako na kisha utamimina na zitakuwa tayari kwa kuuzwa.
NB: ‘Solium benzoate’ hii inapatikana katika maduka ya vyakula, na inasaidia pilipili yako kutowahi kuharibika mapema.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply