Jinsi ya kutengeneza ice cream za ubuyu, ukwaju

Jinsi ya kutengeneza ice cream za ubuyu, ukwaju

Hellow! uhali gani msomaji wangu wa kipengele konki kabisa cha Biashara, bila shaka unaendelea kupambania tonge, leo katika segment hii tupo na dili moja ambalo litasaidia kwa namna moja ama nyingine katika maisha yako.

Kama hujui nini chakufanya basi always segment ya Biashara inajukumu la kuhakikisha msomaji wetu haukosi kitu cha kufanya, katika biashara ambayo watu wengi wanaidharau ni hii ya Ice cream au Lambalamba za tsh 100, lakini hawajui kuwa ndiyo biashara ambayo inalipa zaidi.

Kama kawaida yangu sikuachi mtupu huwa nakusogeza sehemu ambayo unaweza kupata wateja, ukipata sehemu yenye wanafunzi maana hivi ndiyo vitu vyao basi utakuwa umejipata, watu wanadharau tsh 100 lakini ndiyo wengi iliyowakuza.

Wazazi wengi miaka ya nyuma walikuwa wakitegemea kuuza ice cream pamoja na barafu ili kupata kipato, nashangaa sana mtu yupo nyumbani Jokofu lake lipo tu wakati anauwezo wa kuingiza jambo tsh 2000 elf kwa siku, acha kukaa kizembe zinduka wewe.

Mahitaji
• Ubuyu wa unga au ukwaju ½
• Sukari ¾
• Ngano vijiko viwili 2
• Rangi yoyote inayokuvutia ruksaa
• Maji lita 8-10
• Usisahau Vanilla au Hiliki.
Yaani kwa mahitaji yote hayo hayamalizi hata tsh 10,000 elfu, na siyo vitu ambayo unaweza kuvitumia vyote kwa mara moja, mfano rangi au vanilla ni vitu ambavyo unaweza kuvitumia hata mara mbili au tatu.
• Chukua maji yako weka unga wa ubuyu na uhakikishe unga wako wa ubuyu umeuchanganya kabisa na ngano, na uchemshe mpaka uwe mzito kiasi.

Kama utatengeneza Ice Cream za ukwaju basi utaloweka ukwaju wako au kuuchemsha kisha utachuja maji kutoa punje.
• Acha mchanganyiko wako upoe weka rangi, na uanze kuweka katika vifungashio vyake.
Cha kuzingatia naona wengi nitakuwa nimewachanganya kuhusu unga wa ngano lakini ngano inasaidia Ice Cream yako kuwa laini isiwe ngumu, ukitengeneza kwa kutumia unga wa ubuyu au ukwaju tu ice cream yako itakuwa ngumu sana na kama utakosa ngano basi unaweza kutumia Corn Flour.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags