Jinsi ya kusoma message ya WhatsApp kwa siri

Jinsi ya kusoma message ya WhatsApp kwa siri

Awooooteeee!!!! Namna hiyo ndivyo ninavyoanza kwa vibe kama lote mwanangu mwenyewe! Karibu kwenye kipengele kizuri kabisa cha Smartphone, huu ni uwanja wako wakujidai kuimiliki simu yako utakavyo ama nini?

Alright!! Kama kawaida basi wiki hii kwenye smartphone nakuletea njia utakazoweza kuzitumia kusoma message WhatsApp bila mtu mwingine kukugundua, kama unavyojua teknolojia nowadays imekua pana mnoo, acha tufurahie mautundu ya dizaini hii hapa.

Najua wapo baadhi watakua wanafahamu njia hizi lakini acha kukariri na ufuatilie, dondoo hii ya leo hadi mwisho utagundua kitu kipya hapa kwnye hizo njia.

Njia ya Kwanza

Nafahamu kuwa unanijibu ‘aah mbona mimi najua kuondoa last seen kwenye program yangu ya WhatsApp kuna jipya gani?’ Tulia soma hii ili mtu asikugundue kama umesoma text zake, lakini pia vipi na wewe ukitaka kuona message ulizomtumia mtu kama zimefika? Majibu haya hapa.

Unachotakiwa kukifanya ni kusoma message za WhatsApp kupitia notification. Sehemu hii inapatikana juu kabisa kwenye simu yako na hapo ndipo jumbe zote zinapopitia kabla ya kuonekana kwenye program husika.

Unachotakiwa kukifanya ni kuvuta sehemu hiyo ya juu ya pale unapopata ujumbe, kisha bofya sehemu ya replay anza kujibu ujumbe uliotumiwa, kwa kufanya hivyo message itajibiwa bila kuonyesha kama upo online au kama umesoma message hiyo hivyo haitaonyesha kama umesoma message husika.

Njia ya Pili

Hii sasa unatakiwa kupakua program hii hapa inaitwa Unseen- no last Read. Program hii itakusaidia kusoma message za WhatsApp, Instagram, Telegram na mitandao mingine bila kuonekana ‘online.’ Kama wewe ni mmoja watu ambao wanaopenda kusoma message za WhatsApp bila kuonekana basi njia hii ni bora zaidi.

Mbali na kuonekana online pia itakusaidia kuzuia zile tiki mbili za blue ambazo huonyesha kuwa ujumbe umefika na umesomwa.

Yeeeeeeeeeeeeesss!!! Kazi ni kwako kwani kuanzia sasa unaweza kusoma message unazotumiwa bila mtu kugundua kama umesoma. Ulimwengu wa teknolojia ya Smartphone ndiyo mahala pakeee!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags