Jinsi ya kusafisha na kutunza kucha zako

Jinsi ya kusafisha na kutunza kucha zako

Mambo niaje!! My beautifuly people nikukaribishe tena kama kawaida yetu kila weekend lazima tuwe na jambo jipya katika fashion, team Scoop tunakwambia fashion ni usafii mwanetu hakuna mwanamitindo yeyeote duniani ni mchafu.

Leo katika dondoo za fashioni tumekusogezea ni namna gani utasafisha kucha na kuzitunza vizuri kucha zako mwanadada unaependa muonekano mzuri.

Nianze tu na kukuambia hakuna mtu mwenye kucha mbaya niutunzaji tu unatakiwa na mtu bi dada au mtanashati Fulani usichokijua kucha zikiwa safi zinaongeza muonekano, sasa ngoja nikufumbue macho sasa.

Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambavyo utavitumia kwa kusafishia kucha zako unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu.

Kuna watu wanasema kuwa wao kucha zao hata wazitengeneze vipi lakini hakuna maajabu kumbe katika ununuaji wa vifaa hakulinganisha na shape ya kucha zake jamani watu walio tengeneza hivyo vifaa walijua kila mtu ana shape yake ya kucha ndiomaana wakatofautisha.

Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inachangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya.

Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi.

Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, pia napaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi.

Ni vyema kwa mtu anayejali afya na kwendana na fashion ya kucha zake kuchukua muda mwingi kufuatilia kucha zake na kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha zinakuwa katika matunzo mazuri na kujitahidi kubuni mtindo ambao unaweza kuwa tofauti na wengine ambao wanapenda kuzifanya kawaida.

Hata hivyo katika kutunza kucha ziwe nzuri, vyakula ambavyo ni mlo kamili ni muhimu sana, vinginevyo utajikuta ukishauriwa na wataalamu kutumia vitamini mbalimbali kama vile vitamini A, vitamini C, Culcium, Folic Asidi, Protini na Vitamini B12.

Unajiuliza ni kwanini muonekanowakucha zangu ni mbaya kumbe unashindia zako miogo tu kutwa nzima jamani kucha nazo zina hitaji lishe bora hahahahahaha!!

  • JINSI YA KUSAFISHA KUCHA

*Wekeza vifaa vizuri vya kisasa vya kutunzia kucha kwasababu hivyo vifaa vina asali ya chuma so sametimes vinaweza vikaota kutu na kuharibika sasa ukija kutumia haviwezi kufanya kucha zako kuwa na shape nzur.

*Tumia brush ya kucha kwa kusugua chini ya kucha na kuutoa uchafu na kufikia sehemu ngumu ambapo uchafu unajilundika unaweza tumia mswaki ukiwa huna vifaa vya kisasa.

*Tumia maji moto na sabuni ya kunawia mikono ili kuzingatia usafi katika vidole vyako.

*Anza kwa kusugua chini kabisa kwa kushikilia brush chini na sugua kuanzia nyuma kuja mbele pole pole, kisha juu ya kucha fanya hivyo kwa kuzunguka.

*Toa rangi kwa kuloweka pamba kwenye polish remover na usugue kwa vidole vyenye hinna huna haja ya kuitoa. kwa vidole vya afya na nguvu vipumzishe kwa kutumia polish kila baada ya wiki kadhaa.

*Loweka kucha na maji kwenye bakuli, au sinki, au kifaa cha uwezo wako hata dishi poa, kwa maji ya moto ya uvuguvugu na pitisha sabuni ya kunawia mikono. Na ni kucha tu usiloweke mkono mzima,kwa dakika tatu,sabuni kwenye maji hufanya mikono kuwa mikavu .

*Suuza kwa maji ya bomba ya uvuguvugu, au yalokua kwenye chombo yaani jimwagie, kisha zifute na taulo laini.

*Kisha tumia kikatio kucha kukata maana zitakua laini,au kifaa cha kuzipunguza kuweka sawa kama hauzikati.

Asikwambie mtu bhana hakun kitu muhimu kama usafi wa kucha zako na muonekano hii na kukumbusha tena hakuna sababu ya kuacha kucha zako bila muonekano mzuri kwanzia sasa mwanetu, kufikia hapo sisi hatuna laziada tukwambie tu till next weekend.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags