Jinsi ya kupika kachori kwa ajili ya biashara

Jinsi ya kupika kachori kwa ajili ya biashara

Mdogo mdogo ndiyo mwendo ni msemo wa waswahili ambao ni mahususi kwa ajili ya kuwatia moyo wenye nia ya kuanza jambo fulani. Hivyo basi leo tumekusoge biashara ambayo baadhi ya watu wamekua wakiidharau lakini ni kati ya biashara zinazoendesha maisha ya baadhi ya watu.

Licha ya kuwa vitafunwa hivyo huuzwa kwa bei isiyo ghali, lakini wauzaji wake hunufaika endapo wakiitilia maanani. Hivyo basi ili kupata maokoto ya kutosha kila siku biashara hii unatakiwa kuifanya katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vile shuleni na kwenye vituo vya mabasi.

 

Mahitaji

Ili uweze kupika chakula hiki vitu vifuatavyo vinapaswa kuandaliwa:

  • Viazi mviringo (kilo moja au nusu kilo)
  • Unga wa ngano (robo kilo)
  • Pilipili ya unga (kijiko kimoja)
  • Rangi uipendayo kiasi
  • Mafuta ya kupikia (chupa moja)
  • Vitunguu saumu, hoho na chumvi.

Namna ya kuandaa

Menya viazi vyako kisha vichemshe hadi viive kabisa kisha viepue na uweke kwenye bakuli safi na uviponde  hadi vilainike. Lakini hakikikisha viazi vyako havina mabonge bonge.

 

Chukua unga wa ngano, changanya na rangi, pilipili, vitunguu saumu ambavyo tayari vimesagwa na chumvi kwa ajili ya kupata ladha, changanya vizuri na uweke maji kiasi, koroga mpaka mchanganyiko wako utakapo changanyika vizuri, sharti la hapa uji unaokoroga usiwe mwepesi sana wala mzito sana uwe wa saizi ya kati.

 

Baada ya zoezi hilo, chukua viazi vyako ambavyo tayari umeviponda na utengeneza madonge kiasi unachopendelea. Ukimaliza injika karai  jikoni na uweke mafuta na usubiri yapate moto kiasi.

 

Madonge uliyoyaaanda yachovye kwenye unga wa ngano kisha tumbukiza kwenye mafuta ambayo tayari yatakuwa yamepata moto kiasi na kaanga hadi uone ziko tayari na uziepue ili ziweze kuchuja mafuta. Subiri zipoe na uziweke kwenye deli au chombo chochote ulichokiandaa.

Muhimu na kuzingatia katika biashara inayohusisha chakula, hakikisha usafi unaweka mbele, kuanzia wa mwonekano wako hadi chakula unachopika. Siyo mbaya kama utatengeneza na pilipili za kuchombezea kwenye kachori zako






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post