Jinsi ya kupika chipsi za muhogo

Jinsi ya kupika chipsi za muhogo

Habari kijana mwenzangu karibu kwenye kipengele cha Nipe dili kama kawaida leo tutajifunza jinsi ya kupika chipsi za muhogo, karibu tujifunze kwa pamoja darasa hili.

 

Mahitaji


1- Mihogo 5
2- Mafuta lita 1
3.Chumvi kijiko 1cha chakula
4- Chujio
5- Mafuta ya kupikia Lita 1
6- Karai/kaangio

 

Jinsi ya kuandaa


- Menya mihogo yako na ikoshe vizuri

- Chukua kipario cha karoti para mihogo kisha itandaze kwenye sinia na uache zikauke kidogo na Unatakiwa kuziacha saa moja

 

Jinsi ya kupika.


- Weka mafuta kwenye karai acha yapate moto kabisa yaani yachemke yawe makali

- Zigawe mafungu matatu chipsi zako mbichi

- Kisha weka fungu la kwanza kuwa makini mafuta huwa yanakuja juu kwa kuwa Mafuta Ni yamoto sana

- Acha zishikane mpaka chini zipige rangi ya dhahabu

- Geuza chipsi zako upande wa pili acha nao uive vizuri

- Zikiwa tayari zitoe weka kwenye chujio zichuje mafuta

- Acha zipoe kisha zivunje vunje taratibu weka chumvi na Pilipili manga ukipenda

- Unaweza kula na chatne,karanga za kukaanga,njugu za kukaanga au weka kwenye urojo

- Acha chipsi zikauke kabla ya kuzipika ukiweka mbichi zina nyonya mafuta

- Kuwa makini zisiungue kwani zikiungua zinakua chungu na chipsi hizi ni maalumu kwaajili ya kula na Urojo.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags