Jinsi ya kupata marafiki watakaoendana nawewe chuoni

Jinsi ya kupata marafiki watakaoendana nawewe chuoni

Wanachuooooo! Mko wapi mbona siwaoni, nawasalimu kwa jina la university results hahahaha! Nacheka kama mazuri, najua hata wewe unaogopa lakini unajikaza bwana, kama tunavyojua week hizi ni za kupokea matokeo yetu kwa kile tulichokifanya katika semester iliopita, usijali I hope umefanya vyema. 

Kama tunavyojua, wanafunzi wa chuo wanakaribia kufungua chuo, so leo nataka kukujuza jambo bora sana ambalo kama mwanzo ulikurupuka kuchagua marafiki wakati unaingia semester ya kwanza, nataka safari hii uchague waliobora kwasababu darasani kila mtu ushajua tabia yake. 

Mara nyingi chuoni watu hupenda kukutana na watu wapya sio wote. Kuna wale uliokuwa nao shule na mmechaguliwa wote lakini asilimia kubwa huwa wapya.

Kukutana na watu wapya ni jambo zuri na linalotisha kwa wakati mmoja chuoni. Kuna watu wapya utakaoanza nao moja kuwafahamu, utaanza upya kuwa karibu nao, utaanza kuishi nao maisha, na watakuwa kwenye kumbukumbu zako milele.

Ukimaliza chuo kila ukikumbuka maisha yako ya chuo, utakuwa unawakumbuka watu uliochagua kuwa nao ulipokuwa chuoni.

Wakati naenda chuo kuna mtu aliniambia kuwa, watu unaokutana nao chuo unaweza dumu nao muda mrefu kwenye maisha, kwasababu mmekutana nao kipindi uko kwenye ‘the most defining time of your life.’ Lakini pia kama vile mambo mengine kwenye maisha yalivyo na mwanzo na mwisho, sometimes pia urafiki huisha hichi ndo chakukumbuka zaidi.

Chuoni kuna urafiki wa aina tatu:

-Urafiki kutokana na kwamba mpo sehemu moja mfano; mpo course moja, group moja la assignment, room moja hostel nk

-Urafiki kutokana na kwamba mnapenda vitu sawa mfano mnakutana michezoni, kwahiyo mnashtuana kwenda, mnasali pamoja, mimi chuoni marafiki zangu wote tulikuwa tunavaa hijab so tukawa tunaitwa team vijuba, so rafiki anatokana na vit uvipendavyo

-Urafiki kutokana na kwamba mmeamua kuwa marafiki na kuwa there for each other.

Ni kweli kuwa chuoni, kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa marafiki zako, lakini pia kwa vile wengine huigiza maisha ni muhimu kuchagua watu wa kweli kwako, watu unaoendana nao.

Nilikuwa na marafiki wengi chuoni, waliodumu ni wale nilikuwa nimeweka uamuzi kua nataka wawe kwenye maisha yangu, we all need people around us marafiki ni familia unayoichagua wewe mwenyew.


Amua watu unaotaka wakae kwenye maisha yako, and let them know that is what you want. It is important if they feel the same way, ili urafiki usiwe wa upande wako pekee. Naamini utapata marafiki wapya, wachague wale unaoona wanaelekea kule unatamani maisha yako yaelekee.

Kama unapenda kupata marafiki wa kweli chuoni, vitu hivi vitatu vitakusaidia;

  • Be yourself

Kama nilivyosema wengi huigiza jitahidi kua yourself ili upate watu ambao nao hawaigizi, wako vile walivyo, ukiwa sio feki ni rahisi kuona au kujua watu ambao pia hawaigizi maisha.

Usiigize kufanya vitu ambavyo hauvipendi ili tu upate marafiki, utachoka kuigiza Just be yourself, utapata watu watakaokupenda vile ulivyo.

  • Fanya vitu unavyopenda kuvifanya

Ili kupata marafiki mnaoendana fanya vitu unavyopenda kuvifanya wale watu utakaokutana nao huko kuna chance kubwa sana ya nyinyi kuwa marafiki wazuri kwasababu mnashare vitu sawa.

Kwahiyo kama ni michezo, jiunge kwenye timu ya michezo, wachezaji wenzio wanaweza kuwa marafiki zako, kama ni kuimba pia hivyo hivyo.

  • Usitafute kwasababu ya loneliness au kufit in

Watu wengi hutafuta marafiki kwasababu hatutaki kuwa wapweke chukua muda ili upate marafiki kwasababu kweli wanakuletea furaha na wewe unawapa furaha wao na kuwasapoti, kuliko kuwa nao kwasababu tu umpweke na hivyo inabidi uvumilie wanapokufanyia unafiki au kukusambazia habari zako.

Usijaribu kubadilika ili kufit in kwenye kundi la marafiki, be yourself utapata marafiki ambao uko sawa nao.

Yeeeas! I hope tuko pamoja watu wangu kama kawaida yetu yaani ni bandika bandua Mwananchi Scoop hatunaga mba mba mba wala jambo dogo endelea kufuatilia magazine yetu kujifunza Zaidi vitu mbalimbali.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post