jinsi ya kuongeza ufanisi katika kazi

jinsi ya kuongeza ufanisi katika kazi

Mambo vipi kijana mwenzangu? Karibu kwenye jarida lako pendwa ambapo kama kawaida jumatatu ni siku ya makala za kazi, ujuzi na maarifa hapa utapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu kazi karibu.

Ili uweze kuwa bora katika kazi hatimaye upate matokeo chanya unatakiwa kuelewa mambo yatakayokusaidia kuweza kuwa hivyo, Kila kitu unachokiona leo hii mbele ya mboni ya jicho lako elewa kuwa mmliki wa kitu au jambo hilo aliweza kujifunza namna ya kuweza kukifanya kitu au kitu chake kiweze kuwa bora.

Je unafahamu ili uweze kuongeza ufanisi kwenye kazi unatakiwa kufanya mambo gani? fuatilia kwamakini makala haya ili uweze kujifunza mengi.

Unatakiwa kutenga muda wa kujifunza

Hakuna kitu kinachokuwa bora kwa miujiza, kitu chochote ili kiweze kuwa bora ni lazima muhisika wa jambo hilo aweze kuwekeza muda mwingi wa kujifunza juu ya jambo hilo.

Kama unafanya biashara unashauriwa kutoridhika na kile unachokipata pekee, bali ili uweze kupata zaidi unatakiwa kujifunza zaidi ya kuongeza mauzo yako. Watalamu wa mambo wanasema kuwa kujifunza hakuna ukomo, hivyo kwa kila kitu unachokifanya ni vyema ukahakikisha kwamba kwa kila kitu unachokifanya ili kiwe bora na hatimaye upate matokeo chanya huna budi kujifunza kila siku juu ya jambo hilo.

Unashauriwa kujifunza kila kitu kwa sababu hizi ni zama za kisasa mambo yamekuwa yakibadilika sana, pia washindani ni wengi na wanazaliwa kila siku hivyo usipowekeza muda wako mwingi katika kujifunza ni kwamba wewe hautakuwa na utabaki vilevile kila siku hivyo unatakiwa  kujifunza kila wakati ili uweze kwenda sawa na ulimwengu wa sasa.

Jifunze kupangalia kazi zako

Kitu chenye mpangilio ndicho chenye matokeo chanya siku zote, Ili uweze kuongeza ufanisi kwa kila kitu unachokifanya unatakiwa kuelewa namna ya kufanya mpangilio katika kazi zako.

Usikurupe kitandani mwako kama huelewi siku yako itaisha vipi. Bali unatakiwa kupanga ratiba yako katika mtiririko unaoeleweka,  katika hili panga nini unatakiwa kufanya na ndani ya muda gani, kufanya hivi itakusidia sana kuweza kufanya kazi zako kwa wakati pia inakusaidia kutokutoka nje ya malengo yako ambayo umejipangia kuyatekeleza katika siku yako.

Jifunze kuwa mmalizaji wa kazi zako

Kila kitu ili kiwe bora kinatakiwa kumalizika katika kiwango cha ubora. Huwezi kusema unataka kuwa bora katika kazi zako wakati kila kazi unayoianzisha huwa haimaliziki. 

Ukiona unaanzisha kazi fulani halafu  kazi hiyo haimaliki basi ujue hilo hapo kuna shida.

Pindi utakapokuwa na visingizio visivyokuwa vya msingi husasani  katika jambo ulifanyalo elewa kuwa kila kitu unachokifanya kitakuwa kinaishia katika hatua za awali pekee. Hivyo naomba nikusihi ya kwamba kila kitu unachokifanya hakikisha pindi unapoanza kukufanya unakimaliza kitu hicho.

Epuka mrundikano wa kazi

Hili ni jambo la muhimu sana katika ulimwengu wa mafanikio, Kama tulivyoona katika pointi iliyopita basi hapa unashauriwa kuepeuka mrundikano wa kazi, pindi utakapo zipangilia kazi zako basi elewa na namna ya kutimiza kazi kwa wakati ili uepuka mlundikano wa kazi.

Miongoni mwa faida utakazozipata pindi utakapokuwa na utaratibu wa kufanya kazi kwa wakati ni pamoja na kupunguza mrundikano wa kazi ambazo unatakiwa kuzifanya.

Hivyo nakushauri wewe msaka mafanikio ya kwamba unatakiwa kufanya kazi zako kwa wakati ili upate mafanikio ya kweli.

Hakikisha unapata msimamizi.

Kila kitu ili kuweze kuwa bora kinahitaji kuwa na msimamizi, kama unajenga nyumba na huna msimamizi ambaye anaeleweka ni kwamba nyumba hiyo haitakuwa imara. Si kwenye nyumba huo umetumiaka kama mfano tu ila ukweli ni kwamba pindi utakapokuwa na msimamizi bora wa kazi zako utakuwa na maendelo ya kweli. Msimamizi ni mtu muhimu sana katika kila jambo ulifanyalo.

Jiulize maswali

Ili kuwa bora zaidi katika kazi yako ni kwamba unatakiwa kujiuliza maswali, maswali haya ni lazima yalenge ni wapi umetoka, ni wapi ulipo na ni wapi unapokwenda, Kufanya hivi kutakusidia sana kupanga mweleko wa mafanikio yako husasani kile unachokipata.

Wajue washindani wako

Kuwajuwa washindani wako ni njia nyingine ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika kazi zako.  Kuwajua washindani wako inakusaidia sana kujua namna ya kuwashinda  hao washindani  kwa kile ukifanyacho hii ni kwa sababu utakuwa umejua mbinu wanazotumia washindani wako na wewe utakuwa umejua namna ambavyo utawapiku washindani hao.

Mafanikio ni haki yako ya msingi hivyo Ili uweze kupata matokeo chanya  katika kazi yako ni vyema ukahakikisha unayazingatia hayo kila wakati.

I wish you all the best mtafutaji kijana mwenzangu hakikisha unasoma jarida hili kila siku kuanzia j3 hadi ijumaa hakika utajifunza mengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags