Jinsi ya kukabiliana na mazingira magumu kazini

Jinsi ya kukabiliana na mazingira magumu kazini

Na Aisha Lungato

Ooyeeah! Leo kwenye segment yetu ya kazi tunakuletea mbinu ambazo zitakusaidia kukabiliana na kuhimili  mazingira magumu kazini ili yasiweze kukupa stress.

Sio kitu cha ajabu kuchukia kazi yako. Lakini, mara nyingine chuki yako ya kazi haisababishwa na kazi yenyewe, bali watu unaofanya nao kazi na mazingira kiujumla.

 Pia, kuacha kazi papo hapo sio fursa ambayo kila mtu anayo kwa sababu ya gharama kubwa za maisha Tanzania na ushindani katika soko la ajira.

Hivyo unaweza kuta umenasa kwenye kazi usiyoipenda kwa muda mrefu. Sasa, kama una bosi anaye kuonea au wafanyakazi wenzako ni wajeuri, unawezaje kuhimili mazingira magumu ya kazi?

  Weka rekodi ya kila kitu

Kama unafanya kazi na bosi au mfanyakazi mwenza msumbufu, hakikisha mawasiliano yote kati yenu yanafanyika kwa njia ya maandishi kama barua pepe.

Hakikisha unatumia lugha safi na inayoeleweka kwenye nyaraka zote za kitaalamu. Hii itakusaidia hasa, mfano wakati mfanyakazi mwenzako anakutongoza kimapenzi.

Achana na umbea

Usiongeze ukubwa wa matatizo kwa kusambaza habari kuhusu bosi wako au mfanyakazi mwingine ofisini, hata kama wana makosa. Kwa sababu ukishaanza kusambaza habari, na wewe unakua ni sehemu ya tatizo. Pia, si jambo zuri kuchochea wafanyakazi wenzako kuchagua pande za kushabikia, kwa sababu mwishoni inabidi wote mfanye kazi pamoja.

 Omba ushauri kutoka kwa Afisa Rasilimali Watu (HR).

Kama tatizo limekuwa kubwa kiasi kwamba mahala pa kazi si sehemu salama basi wasiliana na HR. Usiogope kutoa taarifa hata kama tatizo linamhusisha bosi wako. Ni wajibu wa HR kuhakikisha kuwa mahala pa kazi ni sehemu salama kwako. Pia, hii ni namna mojawapo ya kuweka rekodi ya tatizo kwa ajili ya kujilinda kama itatokea kesi ya kisheria

Zungumza na mhusika

Inawezekana tatizo lililopo ni sababu ya kuto kuelewana tu. Hivyo ni bora kujaribu kukaa chini na kuzungumza na mhusika uongee upande wako na usikilize upande wake. Hii haimaanishi umshambulie na kumpa mzigo wote wa tatizo yeye, kwani hii itamfanya atake kujilinda. Badala yake, tumia lugha fasaha kama, “Ulivyosema hivi, mimi nilielewa hivi.

Zingatia malengo yako

Mahala pa kazi pagumu panaweza kukufanya usahau kwanini ulikubali kazi hapo mwanzoni. Kama unapenda kazi unayoifanya lakini unakerwa na watu unaofanya nao kazi, elekeza nguvu zako kwenye kufikia malengo yako ya kikazi. Jitihada zako zitakuwezesha kupita vikwazo vyote.

Ebwana eeeh!!! usikose kufuatilia jarida la wiki litakalotoka siku ya ijumaa ili uweze kumalizia madini yako bwana au vipi zingatia mtu wangu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags