Jinsi ya kuanzisha biashara ya vipodozi

Jinsi ya kuanzisha biashara ya vipodozi

Hellow! Watu wangu wa nguvu kama kawaida yetu yani sisi hatunaga mba mba mba, leo katika biashara tunakusogezea mada konki ambayo itaweza kukupa elimu ya kile unachotaka kukifanya, baadhi ya wakinadada wengi wanatamani sana siku moja waweze kufungua maduka ya vipodozi so ungana nasi uweze kufahamu nini ufanye ili ufanikiwe kama wengine.

Biashara ya vipodozi ni miongoni mwa biashara zenye wateja wengi na faida kubwa sana, Ukipata eneo zuri na kuweza kusimamia vizuri biashara yako kuna uhakika wa kuweza kupata faida kubwa zaidi na kupiga hatua kubwa kimaisha.

Biashara ya vipodozi ipo chini ya sheria za mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) na ni lazima kuzingatia taratibu zilizowekwa ndipo uweze kufanya biashara hii kwa amani na uhuru bila ya kusumbuliwa na mtu yoyote.

Kama ilivyo ada siku zote katika kuanzisha biashara lazima uweze kuwa na baadhi ya vitu muhimu kama…

Kama ilivyo kwa biashara zingine biashara hii pia inahitaji eneo maalum (fremu) linalokidhi vigezo vya kuweka duka la vipodozi. Pia utahitaji kuwa na mtaji wa kutosha kuweka mazingira vizuri (mashelfu, kabati nk) pamoja na kununulia vipodozi vyenyewe. Kwa duka dogo la kuanzia basi angalau uwe na Tsh Millioni Tatu (3,000,000/=); na ukitaka duka zuri (la rejareja) basi angalau uwe na Millioni 5 hadi 8.

UTARATIBU WA KUANZISHA BIASHARA YA VIPODOZI

Katika kila biashara kazi lazima kuwe na utaratibu ili uweze kufanikisha jambo lako vile vile katika biashara hiyo kuna taratibu zake nazo ni…

  • Kwanza kabisa pata uhakika wa eneo la kufanyia biashara na mkataba (kama eneo ni la kupanga) au hati ya umiliki (kama eneo ni la kwako). Baada ya hapo nenda mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN).
  • Ukishapata TIN sasa nenda mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) katika ofisi ya kanda iliyopo karibu na wewe kwa ajili ya kusajiliwa na kupewa kibali cha kufanya biashara ya vipodozi.
  • Ukishapata kibali cha TFDA sasa piga photocopy na uende manispaa kwa ajili ya kupata leseni ya biashara.

Baada ya kupata TIN, kibali cha TFDA na leseni ya manispaa unapotaka kuanzisha biashara yako sasa unaruhusiwa kuanza biashara yako.
Sasa unaweza kununua vipodozi kutoka maduka ya jumla na kuweka dukani kwako. Cha muhimu kuangalia kabla hujanunua bidhaa zako inabidi kutazama expire date za bidhaa hizo ili kuepuka kuwauzia watu bidhaa zisizo tumika.

I hope umeelewa vya kutosha mtu wangu wa nguvu sisi jukumu letu ni kukuelimisha wewe ambae unandoto ya kufanya jambo fulani lakini unaogopa kwasababu ya meneno ya vitisho ya watu, so mpaka hapa ushaelewa nini ufanye ili uweze kumiliki duka lako la vipodozi, fanya maamuzi sasa naamini utafanikiwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags