Jinsi bamia inavyoondoa chunusi usoni

Jinsi bamia inavyoondoa chunusi usoni

Habari msomaji wetu wa mambo ya fashion, ni siku nyingine tena tunakutaka hapa ili kuweza kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala mitindo, urembo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua tu zaidi.

Leo bwana kwenye ukurasa wetu huu wa  masuala ya urembo tutaangalia juu  ya mboga aina ya bamia jinsi inavyotibu chunusi na kuziondoa moja kwa moja usoni.

Mboga hii mbali na kuondoa chunusi usoni, pia husababisha ngozi kuteleza na kuwa nyororo.

JINSI YA KUFANYA

Chukua bamia zikatekate vipande, ziweke kwenye brenda kisha chukua limao kipande na maji kidogo, weka kwenye brenda kisha saga.

Baada ya kupata mchanganyiko wako upake usoni mpaka kwenye shingo, acha kwa muda ikauke kisha bandua kama unavyoondoa maski nyingine usoni.

Fanya hivyo kwa siku tatu kwa wiki itakusaidia kuondoa kabisa chunusi usoni.

Aidha bamia zina uwezo wa kuondoa bakteria usoni na muwasho wa aina yoyote kwenye ngozi. Kama utatumia kwa muda huo utakuwa na ngozi nzuri.

Ila Kumbuka: Usitumie tiba hii kama una tatizo la ngozi au kama una vidonda vyovyote usoni kwani itakusababishia matatizo makubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags