Aliyekuwa gwiji wa soka marehemu Edson Arantes do Nascimento, maarufu kama Pele, jina hilo limeingizwa rasmi kwenye kamusi likimaanisha kitu ama jambo la "kipekee kisicholinganishwa".
Kamusi ya Michaelis ya lugha ya Kireno, ni moja ya kamusi maarufu zaidi nchini Brazil, iliongeza "pele" kama kivumishi kipya.
Kuingizwa kwa jina lake kwenye kamusi kulikuja baada ya kampeni ya Pelé Foundation ya kumuenzi nyota huyo wa kandanda kukusanya saini zaidi ya 125,000.
Ikumbukwe tu Pele alifariki mnamo Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 82. Gwiji huyo wa pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, anachukuliwa kuwa mwanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani na katika historia.
Chanzo BBC
Leave a Reply