Jina la kanumba bado linaishi

Jina la kanumba bado linaishi

Wakati akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kuzunguka mataifa mbalimbali mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny akiwa South Africa amekutana na shabiki wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba ambaye alieleza kuwa kwa Tanzania anamumkubali zaidi muigizaji huyo.

Kupitia Instastory yake Rayvanny ame-share video ya shabiki huyo ambaye alikuwa akimuuliza swali ni muigizaji gani ambaye anamkubali zaidi nchini Tanzani ambapo alijibu kuwa ni  Marehemu Kanumba.

Aidha kupitia video hiyo Rayvanny alitumia wasaa huo kuwashauri waigizaji wa bongo movie kuendelea kupambana kwani kazi zio zinafika mbali.

Marehemu mwigizaji Steven Kanumba alifariki April 7, 2012 akiwa na miaka 28, ambapo alitamba na filamu zake mbalimbali zikiwemo

‘Magic House’, ‘Off Side’, ‘Moses Never Say Never’, ‘Kijiji cha tambua haki’, ‘Bigg Daddy’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags